Posted: 2023-09-27
Kwa mujibu wa ibara ya 25(a) ya katiba ya Chama cha Watakwimu Tanzania (TASTA), Mkutano Mkuu kwa mwaka 2023 utafanyika tarehe 26 na 27 Oktoba 2023 katika Ukumbi wa Venance Mabeyo, Jijini Dodoma. Mkutano utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Venance Mabeyo kuanzia saa 2:30 asubuhi. Wanachama wote mnaalikwa na kuhimizwa kuhudhuria mkutano huu wa kikatiba. Tafadhali thibitisha ushiriki kupitia info@tastastat.or.tz.